Mawakili kumi wafa ndani ya miezi miwili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimepoteza wanachama wake zaidi ya 10 katika kipindi cha miezi miwili, idadi ambayo haijapata kutokea tangu nchini.


Vifo vya mawakili hao ambao wamefariki kati ya Desemba 2020 na Januari 2021 kwa maradhi mbalimbali wakiwamo wawili waliofariki Ijumaa na Jumamosi mkoani Morogoro, vinaonekana kuitikisa jumuiya hiyo.



Ingawa mawakili wenyewe kupitia makundi yao katika mitandao ya kijamii yakiwamo ya Whatsapp wamekuwa wakitoa hisia zao kutokana na kile kilichosababisha vifo vyao, lakini hakuna taarifa rasmi ya vifo mfululizo vya wenzao.



Kwa mujibu wa orodha ambayo gazeti hili limeipata kwa kushirikiana na uongozi wa TLS, ni mawakili wawili wa mkoani Morogoro, Alex Sikalumba na Allen Mwakyoma waliofariki Ijumaa na Jumamosi ya wiki iliyopita.



Wengine ni Angel Korosso aliyefariki Januari 28, Edson Mkisi aliyefariki Januari 26, Lord Munuo Ng’uni aliyefariki Januari 25, Profesa Nicholaus Nditi aliyefariki Januari 27, Tumaini Pius aliyefariki Januari 21 na Hashim Ngole Januari 9.



Mikoa iliyotikiswa na vifo hivyo vya mawakili wa kujitegemea ambao ni wanachama wa TLS ni Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tabora, Dodoma, Morogoro na katika orodha ya mawakili waliokufa yuko pia Aneth Lwiza.



Wakili wa kujitegemea wa mjini Moshi, David Shillatu alisema matukio ya vifo mfululizo miongoni mwa mawakili ni ya kuogofya na haijawahi kutokea hivi tangu Tanzania ipate uhuru wake.



“Ni matukio ya kuogofya kidogo na niseme kwa kweli hayajawahi kutokea hata kama sasa jumuiya ya mawakili leo ni kundi kubwa kidogo, lakini hivi ni vifo vya mawakili wengi kwa mfululizo tangu nchi ipate uhuru,” alisema Shillatu.



Wakili mwingine, Patrick Paul alisema vifo hivyo mfululizo vya wenzao vinawapa wasiwasi lakini kwa asili ya kazi yao wanakutana na watu wengi na kushika nyaraka zilizopitia mikono ya watu wengi.



“Siwezi kusema huyu amekufa na ugonjwa huu au ule lakini kwa `nature’ (aina) ya kazi yetu tunakutana na watu wengi na kushika nyaraka nyingi, huwezi kubaini nani ana ugonjwa wa kuambukiza,” alisema.



Patrick alisema pamoja na wao sasa kuhakikisha wanachukua tahadhari za kiafya, lakini pia mawakili wengi si watu wa mazoezi na hiyo husababisha kupata maradhi kama ya kisukari, moyo na shinikizo la damu.



Rais TLS afunguka

Akizungumza na gazeti hili kuhusu vifo hivyo, Rais wa TLS, Dk Rugemeleza Nshala alisema wanachama zaidi ya 10 wamefariki ndani ya miezi miwili wakati wiki iliyopita pekee, chama hicho kilipoteza wanachama wanne.



Dk Nshala alisema wanachama hao wamefariki kwa sababu tofauti kama vile ugonjwa wa sasa wa homa kali ya mapafu pamoja na magonjwa mengine yasiyoambukiza kama vile kisukari, figo na shinikizo la damu.



“Ni pengo kubwa katika tasnia ya sheria kuondokewa na wanachama wengi. Tunapita katika kipindi kigumu. Wiki iliyopita tulimpoteza Profesa Mbiti na wiki moja kabla tulimpoteza Profesa (Josephat) Kanywanyi,” alisema.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad