Msanii wa filamu aonyesha operesheni ya urembo ilivyoharibu pua yake

advertise here


Beijing, China (AFP). Mcheza filamu wa kike wa China ametuma picha yake mtandaoni akionyesha jinsi pua yake ilivyoharibika baada ya kufanyiwa upasuaji ili kuongeza urembo.


Msanii huyo, Gao Liu ameonya mashabiki wake kuhusu operesheni hizo.Katika picha aliyotuma mtandao wa Twitter inayoonyeshas sura yake baada ya operesheni hiyo, pua yake ina alama nyeusi kutokana na tishu za eneo hilo kufa.Aliwaandikia wafuasi wake milioni tano alisema hisia alizonazo baada ya kuharibika huko kwa muonekano wa pua yake ni za kujiua na suala hilo limempotezea kazi nyingi za uigizaji."Nilidhani awali kuwa masaa haya manne ya upasuaji yangenifanya niwe mzuri zaidi, lakini sikutambua kuwa yatakuwa mwanzo wa ndoto mbaya," aliandika Jumanne.Upasuaji wa kurekebisha mwili unakua nchini China, huku watu milioni 15.2 wakikadiriwa kuwa wamefanyiwa operesheni mwaka jana, kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya utafiti ya iiMedia.Gao alisema alitegemea upasuaji huo ungeboresha fani yake ya uigizaji.Lakini anasema alichodhani ni mabadiliko madogo ya kuweka tishu mbele ya pua mwishoni mwa mwezi Oktoba, lakini ikaathirika, na hivyo kuhitaji upasuaji zaidi, aliandika.Gao alisema baadaye alilazwa hospitali kwa siku 61 na hivyo kupoteza dola 61,000 za Kimarekani (zaidi ya Sh140 milioni) kazini.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE