Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Utata juu ya kifo cha dereva Mbeya wapatiwa majibuKamati  ya kuchunguza utata ulioibuka kuhusu mazingira ya kifo cha aliyekuwa dereva wa lori, Abdulhman Issa  imebaini kuwa dereva huyo hakupigwa na Askari wa kikosi cha usalama barabarani kama ilivyoelezwa hapo awali.Kamati hiyo iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya RC Albert Chalamila imebaini kuwa dereva huyo amefariki akiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Igawilo iliyopo  jijini Mbeya.
RC Chalamila ametoa ripoti hiyo mbele ya  waandishi wa habari  leo  na kueleza   kuwa marehemu Issa alianza kujisikia vibaya akiwa njiani kabla ya kulazwa katika hospitali ya Mision Chimala ambapo alibainika kuwa na homa kali ya mapafu (Pneumonia).
Aidha Baada ya ripoti hiyo Chalamila ameruhusu mwili wa marehemu kuzikwa na kuagiza  Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kugharamia gharama zote za mazishi  kwa kushirikiana na familia ya marehemu Issa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments