Wanaume wanaongoza kufariki kwa UKIMWI kuliko wanawake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Imeelezwa kuwa wanaume wenye Virusi vya UKIMWI (VVU) wanaongoza kwa kufa kutokana na kusuasua kunywa dawa za kufubaza virusi hivyo ikilinganishwa na wanawake.


Akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibitibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko, amesema wanaume wamekuwa nyuma katika kupima UKIMWI na wanaojitokeza kupima wanapobainika kuwa na maambukizi wamekuwa hawanywi dawa hizo na hivyo hufariki.


Amefafanua kuwa takwimu za mwaka 2019 zinaonesha kuwa wanaume wanaoishi na VVU ni 628,830 huku wanawake ni 983,471. Hata hivyo, amesema vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa wanaume ni 12,225 huku wanawake ni 9,304.


DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Amesema idadi ya wanawake wanaokufa ni ndogo kutokana na kuzingatia masharti ikiwamo kuanza kunywa dawa mapema pindi wanapobainika kuwa na ugonjwa huo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad