Azam FC Wafunguka Kuishusha Yanga Kileleni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utatumia mpango wao wa kutumia faida ya matokeo mabaya ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kwa lengo la kuwaondoa kileleni.

Azam yenye pointi 44 wapo nyuma ya Yanga wenye 50 wakitofautiana idadi ya michezo waliyocheza yenyewe ikiwa mbele kwa 24 na wapinzani wao 23.

 

Timu hizo zote zimepania kubeba taji hilo katika msimu huu unaotetewa na Simba ambao wenyewe wapo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 46.

 

Akizungumza na Champio-ni Jumatano,Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema kuwa kabla ya kuanza kwa msimu walijiwekea malengo na kubwa ni kubeba ubingwa wa ligi msimu huu.



“Tangu mwanzoni mwa msimu huu tuliweka wazi kuwa tuna jambo letu, na hii ni katika kuhakikisha tunajitahidi kumaliza nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi.

 

“Hivyo, hatuna presha na mtu aliye nyuma yetu, bali sisi tunamwangalia aliye juu yetu, na kwa sasa Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi, hivyo malengo yetu ni kujitahidi kushinda michezo iliyo mbele yetu ili kupunguza pengo la pointi lililo kati yetu.“

 

Uzuri ni kwamba Yanga nao hawajawa na mwendelezo mzuri na wameangusha pointi nyingi, hivyo ni jukumu letu kulichukulia hilo kama faida na kuwakaribia au hata kuwazidi.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad