Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Bilionea wa Kijapan anawatafuta watu wanane wa kupaa nao hadi mwezini

 


Bilionea wa Japan Yusaku Maezawa amewakaribisha watu wanane kutoka kwa umma kujiunga nae kwa ajili ya safari ya kuutembelea mwezi katika chombo cha anga za mbali cha Elon Musk SpaceX .

"Ninawataka watu wa matabaka mbali mbali kujiunga nami ,"aisema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, ambako pia alitoa maelezo ya maelezo ya maombi kwa wale wanaotaka kwenda kupitia kiunganishi hiki shared a link to application details.


Amesema atalipia ghara zote za safari hiyo, kwahiyo wale watakaosafiri nae katika chombo hicho watasafiri bure.


Maombo yanahitaji waombaji wawe wametimiza vigezo viwili: wawe na malengo ya "shughuli yoyote" ambayo wanaifanya "kuwasaidia watu wengine na jamii bora kwa njia fulani ", na wawe tayari "kujitolea kusaidia wasafiri wengine ambao wana maono yanayofanana na yao ",alisema:


"Nimenunua viti vyote, kwahiyo itakuwa ni safari ya kibinafsi ," aliongeza.


Bw Maezawa, ambaye ni mwanamitindo maarufu na mkusanyaji wa sanaa, awali alisema anapanga kuwaalika "wasanii" kwa ajili ya safari katika roketi ya Starship, lakini mradi wake uliofanyiwa marekebisho "utawapatia watu kutoka maeneo mbali mbali ya dunia fursa ya kujiunga na safari yake ".


"Kama unajiona kama msanii, basi wewe ni msanii ," alisema.


Mwaka jana, pia alizindua kipindi cha kuwasaka marafiki wa kike kujiunga nae katika safari, kabla ya kuifuta kutokana na ''hisia mchanganyiko''

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments