Dkt. Magufuli ameliacha taifa na heshima kubwa- Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ameliacha taifa likiwa salama na heshima kubwa sana.
Hayo ameyasema akihutubia wananchi wa Chato ambao leo wanaaga mwili wa Hayati Magufuli na kusema kuwa Hayati Dkt. Magufuli aliaacha alama katika kila sekta hivyo hata siku moja haiwezi kutosha kuchambua jinsi alivyolitumikia taifa.

“Dkt. Magufuli ameliacha taifa hili likiwa salama na likiwa na heshima kubwa sana, tuliona alitutoa kwenye uchumi wa chini hadi uchumi wa kati kabla ya muda ambao ulitabiriwa na wataalamu na ni heshima kubwa sana heshima yake itaendelea kukumbukwa ni wajibu wetu viongozi na Watanzania tuungane kuyaenzi yale mazuri yote,” amesema Mhe. Abdulla.

Pia Mhe. Abdulla amesema Hayati Dkt. Magufuli alikuwa na maono makubwa hivyo hakuna mtanzania ambaye hajaumizwa na kusikitishwa na msiba huu mzito lakini kama bindanu inawapasa kukabiliana nalo na waweze kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

“Dkt Magufuli alikuwa na maono makubwa kiasi kwamba hakuna mtanzania mwenye akili timamu ambaye ndani ya damu yake, na ya mioyo yake hakusikitika na jambo hili kwa kweli ni jambo zito, lakini lazima kama binadamu tuweze kukabiliana nalo na tuweze mstiri na kumpeleka kwenye nyumba yake ya milele kwa heshima,” amesema Mhe. Abdulla.

Aidha, amewahakikishia wananchi wa Chato kuwa watapata fursa ya kuaga mwili wa Hayati Dkt. Magufuli na hawatauzungusha mwili wa Hayati Dkt. Magufuli kwa gari kama walivyofanya kwenye baadhi ya maeneo hivyo kuwasisitiza kuwa watulivu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad