Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar awatembelea majeruhi wa ajali “Imenibidi kusitisha ziara yangu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






Na Thabit Madai, Zanzibar.
GARI ya Waandishi wa Habari waliokuwa katika Msfara wa Mkamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Sueiman Abdul imepata ajali katika eneo la Mtule Wilaya ya Kusini wakati wakielekea katika Ziara ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika Ajali hiyo jumla ya watu wanne (5) wamejeruhiwa vibaya huku mwandishi mmoja anaejulikana kwa jina la Khamis Ali Khamis miaka 64 amefariki hapo hapo ambapo majeruhi wa ajali hiyo wakikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.

Majeruhi hao ni pamoja na Kassim Abdi Hassan (35) Abdulrahim Khamis Mussa(25) Hassan Issa Mwadini (59) Abdullah Khamis Ali (30) Abdulwahid Suleiman Yussuf (26)

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa Tatu na Nusu asubuhi ambapo ajali hiyo ilihusisha gari Nne, mbili zikiwa za binafsi na gari mbili za Serikali ambazo zilikuwa katika msafara huo,” alisema.

“Gari Nne 4 zimehusika katika ajali hiyo ambapo gari aina ya Alphad iliyokuwa inatokea Shamba kwenda Mjini  iliingilia msafara huo wa Makamu wa Pili wa Rais na kusababisha gari mbili  prado ambazo zilikuwa k msafara huo kupata ajali pamoja na gari aina ya Rava Z 178 KT ambayo ilikuwa inaendeshwa na mgeni raia wa Romania Salina Flava miaka 24,” alisema

Kamanda alisema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya kutokea kwa jail hiyo huku maejeruhi wote wakiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mazi Mmoja Mjini Unguja.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kwenda kuwatembelea majeruhi wa ajali hiyo, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdul alipongeza juhudi zilizochukuliwa na Madaktari katika hospitali ya Mnazi mmoja katika kuwapoke na kuwahudumia majeruhi wa ajali hiyo.

“Imenibidi kusitisha ziara yangu katika Mkoa wa Kusini Unguja mara baada ya kutokea kwa ajali hii ambapo tunawaombea kwa mungu wale wapone wale ambao wameata meraha huku Mwenyezmungu amlaze mahali pema peponi alietngulia mbele ya haki,” alisema.

Majeruhi wa ajali hiyo wamefikishwa katika hospitli ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa matibabu zaidi ambapo Viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi walikwenda kuwakagua majeruhi wa ajali hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad