Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mbunge Sanga aipigia magoti serikali juu ya kusua sua kwa shamba la ng'ombe la kitulo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMbunge wa Makete Ndg Festo Sanga ameiomba serikali kuligeukiwa shamba la Maaalum la kitulo la Ng'ombe wa maziwa ambalo lilianzishwa na Mwl Kambarage Nyerere kwaajili ya kuzalisha maziwa kwaajili ya Viwanda vya Tanzania na Watanzania.

Shamba la Kitulo ndio Shamba pekee kwa ukanda wa Africa Mashariki lenye ng'ombe wanaotoa lita 40-50 kwa siku, lakini kwa muda mrefu limekuwa halikui na ng'ombe hawaongezeki.


Sanga ambaye alifanya ziara ya kukagua shamba hilo, amemuomba Mh Rais na Wizara husika kuchukua hatua za Maksudi kuhakikisha shamba hili linakuwa na tija ambayo Mwl.Nyerere aliiiona, hasa ikiwa ni kuzalisha maziwa ya kutosha kwa watanzania wote.


Kwa sasa Shamba halina vifaa vya kisasa vya kuendeshea shughuli za shamba, lakini majengo ni chakavu, na idadi ya mifugo imekuwa ikipungua badala ya kuongezeka.

Post a Comment

0 Comments