Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Muuguzi Afukuzwa Kazi kwa Kubaka Mwanafunzi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa Tabora, limeazimia kufukuzwa kazi aliyekuwa Muuguzi wa zahanati ya Kalunde, Elipidius Kweyamba, baada ya kupatikana na hatia ya kubaka mwanafunzi na kumpa mimba.

 

 

Akitangaza maamuzi ya Kamati ya Nidhamu katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika jana Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Ramadhan Shaban Kapela alisema wamefikia hatua hiyo baada ya mtumishi huyo kupatikana na hatia ya kubaka hivyo kuhukumiwa na mahakama miaka 30 jela.

 

 

Alisema kuwa hukumu hiyo ilitolewa mwezi Septemba mwaka jana baada ya mtumishi huyo kupatikana na hatia ya kumwingilia kwa nguvu kimapenzi mwanafunzi na kumpa ujazito.

 

 

“Baraza limeafiki kufukuzwa kazi Muuguzi huyo baada ya kujiridhisha kuwa alikiuka maadili ya utumishi wa umma na hata baada ya kusomewa hukumu hakukata rufaa kama sheria inavyoeleza, hivyo tumemfukuza kazi rasmi,” alisema.

 

 

Aidha, Mstahiki Meya aliongeza kuwa mtumishi mwingine Rehema Magaiwa Mussa (Muuguzi katika zahanati hiyo) amesamehewa na kurejeshwa kazini na atakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miezi 6 baada ya kupatikana na hatia ya kutofika kazini kwa siku 37.

Post a Comment

0 Comments