Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Pyramids yaichapa Namungo Kombe la Shirikisho barani Afrika

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika klabu ya Namungo FC, imepoteza mchezo wa pili mfululizo wa kundi D’ kwa kufungwa mabao 2-0 na Pyramids ya Misri.
Mabo ya Pyramids yamefungwa na Ramadhani Sobhi dakika ya 71 kwa mkwaju wa penati, na mnamo dakika ya 84 Omar Gaber akaipatia timu hiyo bao la pili, kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Ushindi huu wa Pyramida unawafanya wafikishe alama 6 na kuendelea kusali usukani mwa kundi D’ baada ya kushinda michezo miwili, mchezo wa kwanza waliifunga Nkana mabao 3-0, baada ya kipigo hiki cha pili mfululizo Namungo sasa wanaburuza mkia wakiwa haawana alama hata moja, baada ya mchezo wa kwanza kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Raja Casablanca.

Mchezo mwingine wa kundi hili unachezwa majaira ya Saa 1-0 Usiku ambapo Nkana ya Zambia watakuwa wenyeji wa Raja Casablanka ya Morocco.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments