Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Thierry Henry Ajiondoa Katika Mitandao ya Jamii Kisa Ubaguzi wa Rangi


Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa, Thierry Henry (43) amejiondoa kwenye mitandao yote ya kijamii kutokana na ongezeko la visa vya ubaguzi wa rangi katika majukwaa hayo.

Henry ambaye alikuwa na wafuasi milioni 2.3 kwenye mtandao wa Twitter amesema visa vya ubaguzi wa rangi mitandaoni vimefikia kiwango cha kutisha kiasi cha kutopuuzwa tena. Kwa mujibu wa Henry, hatarejea tena kwenye mitandao ya kijamii mpaka Kampuni zinazomiliki majukwaa hayo zitakapoanza kukabiliana na suala la ubaguzi wa rangi kwa kiasi sawa na jinsi wanavyopigana na tatizo la kukiukwaji wa haki miliki.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments