Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Utata Waibuka Mimba Amber Lulu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Utata mzito umeibuka juu ya mimba aliyobeba msanii wa bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ ambapo swali la msingi la wengi ni nani baba wa mtoto au mwenye ujauzito huo?

 

Katika mahojiano yake na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA wakati wa baby shower yake iliyofanyika katika Ukumbi wa Hekima Garden uliopo Mikocheni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Amber Lulu alisema hata yeye hajui baba wa mtoto au aliyempa mimba hiyo.“Hata mimi simjui baba wa mtoto,” alisema Amber Lulu akiomba waandishi wamwache kwani anahitaji hewa.

 

Kufuatia jibu hilo ndipo wenye kujua ishu kwa undani wakaling’ata sikio Gazeti la iJuMaa WikiENda kwamba, Amber Lulu hatanii, bali ni kweli hajui ni nani mwenye mimba hiyo.Kwa mujibu wa watu wa karibu, ni kweli anachokisema Amber Lulu kwa sababu hata yeye mwenyewe anashindwa kutengua kitendawili hicho kigumu.“Unajua wakati anapata ujauzito, Amber Lulu alikuwa na uhusiano na watu wawili; mmoja ni msanii wa Bongo Fleva na mwingine ni mtayarishaji mkubwa wa muziki Bongo “

 

Unajua hata Amber Lulu anapata utata huohuo kwa sababu wakati ule alikuwa kwenye uhusiano na huyo msanii, lakini alikuwa akichepuka na huyo prodyuza wa muziki na hata mke wa huyo prodyuza anajua kwa sababu kuna siku alimpigia simu akamchapa sana.

 

“Inawezekana siku alipopata mimba, mchana alikuwa kwa boyfriend wake ambaye ni huyo msanii mzuri tu wa Bongo Fleva hivyo walifanya tendo na baadaye labda alikutana na huyo prodyuza wakafanya yao.“

 

Huyo msanii kwa sasa ana uhusiano wake na mwanamama wa Bongo Movies na huyo prodyuza naye ana ndoa yake hivyo kila mtu haelewi nini kinaendelea au ni nani hasa atakubali kulea mtoto atakayezaliwa,” anasema rafiki wa karibu wa Amber Lulu.

 

Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta Amber kwa mara nyingine kwa njia ya simu na kumtajia wanaume hao wawili wanaotajwa kumpachika ujauzito huo, aliwakataa wote.“Siyo huyo…(anataja jina) wala huyo (anataja jina la msanii),” alisema Amber Lulu kisha akakata simu.

 

Hadi sasa, ujauzito wa Amber Lulu una zaidi ya miezi nane hivyo anasubiria kujifungua baada ya kutimiza miezi tisa.

Post a Comment

0 Comments