Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Yanga SC yatoa sare Arusha, Yondani Red Card

 


Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Yanga umemalizika kwa sare kwenye uwanja wa Sheikh Abeid jijini Arusha.

 

Sare hiyo imepatikana baada ya Polisi Tanzania kusawazisha dakika za mwisho wakiwa pungufu, kufuatia mlinzi wao Kelvin Yondani kuoneshwa kadi nyekundu.


Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 41 kupitia kwa Fiston Abdoulrazak ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kelvin Yondani (kushoto) na Fiston Abdoulrazak wakiwania mpira


Kipindi cha pili timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini matumizi ya nafasi hayakuwa mazuri hadi dakika ya 87 Kelvin Yondani alipooneshwa kadi nyekundu kisha dakika za mwisho kabisa Polisi Tanzania wakasawazisha kupitia kwa Pius Buswita.


Yanga SC imefikisha pointi 50 kwenye mechi 23 ikiwa mbele ya Simba SC yenye pointi 45 kwenye mechi 19.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments