Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Bashungwa angilia kati suala la kushikiliwa wanahabari
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, ametangaza rasmi kufuatilia suala la Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke, Lusabilo Mwakabibi kutoa amri ya kukamatwa na kuweka chini ya ulinzi kwa muda wa masaa matatu wanahabari jijini Dar es salaam.

Tukio hilo lililotokea Wilaya ya Temeke siku ya jana Aprili 12, 2021 baada ya wanahabari kuhudhuria mkutano wa Mkurugenzi wa Wilaya ya temeke, Mwakabibi Pamoja na wafanyabiashara.

Waziri Bashungwa amewataka waandishi wote wa Habari na wale wanadai kutendewa kitendo hicho kuwa na Subira katika suala hili na kutoa ahadi ya kulifanyia kazi.

“Tunafuatilia malalamiko ya wadau wa tasnia ya habari juu ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi wanahabari wetu.

“Tunaomba wanahabari wawe na subira wakati tunalifanyia kazi suala hili.” alisema Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Bashungwa.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments