Mambo 10 nilioyaona Mwadui vs Simba
1: Football At its Best🙌 Zimepigwa dakika 90 za akili, hofu na mipango mingi. Haikuwa perfomance nzuri kutoka kwa Simba lakini mwisho wa siku wameondoka na pointi 3 muhimu kwenye begi lao
2: Kwa benchi la Ufundi na wachezaji ww Mwadui.. Thank you very much👏 Wametupa mechi nzuri ya kutazama kwa kukubali kuwa 'watumwa' kiwanjani. Walijitoa sana kukimbia maeneo mengi ya uwanja na kuwapa Simba mtihani mgumu wa kujibu
3: Simba walianza mechi kwa tempo ya chini kiasi. Ni kama nafasi ya Mwadui kwenye msimamo iliwafanya warelax kidogo. Kadiri dakika zilivyokuwa zinazidi kukimbia ndio kengele ya hatari ikaanza kugonga vichwani mwao
4: System ya Da Rosa (4-2-3-1) ilikuwa sahihi kwenye makaratasi lakini kwa hali ya uwanja wa Kambarage ile pacha ya Mkude na Nyoni ilikosa nguvu ya kuisukuma zaidi timu mbele
5: Well Done kocha wa Mwadui.. Hii mechi walijiandaa zaidi kisaikolojia. Ile 'Low Block Defensive system' waliicheza kwa umakini mkubwa sana. Kwa 'Mentality' ya leo ni ngumu sana kuamini kama hii ni timu inayoburuza mkia
6: Joash Onyango🙌 NUSU MTU, NUSU CHUMAA. Mwamba kweli kweliii. Viwanja vigumu kama vile vinahitaji watu wagumu kama Onyango kuvimudu. Alikuwa bora hewani, akawa bora kuzuia njia za 'kaunta' za Mwadui
7: Larry Bwalya.. Hesabu za mpira zimelala kwenye ubongo wake. Aligusa na kuachia mpira haraka kwenye nafasi. Viungo wa Mwadui 'walienjoy' kuwa karibu na Chama sio Bwalya
8: William Lucian 'Gallas'🙌 Leo amenikumbusha mapafu yake kwenye kuusaka mpira kama mbwa anavyosaka mnofu kwenye chumba cha kiza.. Alikuwa bora sana kwenye kukaba na kuanzisha mashambulizi. Changamoto pekee iliyomsumbua ni uwezo wake wa kupiga pasi ndefu sahihi
9: John Bocco💪 Dhidi ya mabeki wagumu, kiwanja kigumu mpe Bocco hiyo shughuli aimalize kwa bao gumu. Ni aina ya mabao muhimu ambayo ni nadra sana kuyaona yakikumbukwa mwisho wa msimu
10: Uhuru Selemani alikuwa na mechi yake mkononi. Alijitoa na kujituma sana. Shukrani sana Kapombe kwa mechi nzuri
Nb: Kwa pumzi ile .. Tar 8 Ambulance ziongezwe 😀