Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mobeto Ampora Wema Sepetu Duka

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
ILE fremu ya duka ambayo ilikuwa likimilikila Staa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu imedaiwa kumilikiwa na staa wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto kwa sasa, RISASI limefatilia.Duka la hilo la nguo za watoto lililokuwa likimilikiwa na Wema maeneo ya Mwananyamala Komakoma, Kinondoni jijini Dar, lilikuwa likijulikana kwa jina la Little Sweetheart.Kwa sasa limebadilishwa jina na kuwa Mobeto Kids Corner.


Awali, tetesi zilivuja kwamba Wema ameshindwa kulipa kodi hivyo mwenye nyumba anamtaka ahame ili apangishe mtu mwingine.Wakati mambo bado yapo motomoto, ghafla Mobeto akaposti duka hilo kupitia akaunti yake ya Instagram na kuandika kuwa amenunuliwa na mpenzi wake na kuwekewa kila kitu ndani hivyo wanachokisubiri ni muda tu wa kuanza kuuza bidhaa zao.


“Mh! Jamani mbona hili duka ni kama lile alilokuwa anamiliki Wema? Kwani imekuwaje tena hadi Mobeto naye ameanza kulimiliki? Ila hawa mastaa wana visa jamani, kwa hiyo aliona mwenzake anafaidi kuuza pale akaona amfanyie mtima nyongo…” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maggie.RISASI KAZINIIli kupata ukweli wa mambo yote hayo RISASI lilifunga safari mpaka eneo lilipo duka hilo na kufanikiwa kujiridhisha kwamba awali lilikuwa duka la Wema na sasa ni linamilikiwa na Mobeto.

“Ni kweli mwanzo hili duka lilikuwa linamilikiwa na Wema lakini sijui kilitokea nini akaondoka ndio Mobeto akaja kulichukua,” alisema dada mmoja aliyejita mbulisha kuwa ni mfanyakazi wa Mobeto.


“Sisi wenyewe wakati Mobeto anakuja hapa kuangalia duka lake tulishangaa kwa sababu mwanzo alikuwa Wema tena kilicho tushangaza zaidi ni kuwa na yeye anauza nguo za watoto kama alivyokuwa akifanya mwenzake, sasa sijui kwa nini imekuwa hivi,” alisema jirani mmoja kwa sharti la kutotajwa jina.


NDUGU WA MMILIKI AZUNGUMZARISASI pia lilizungumza na kijana mmoja aliyejitambulisha kuwa ni ndugu wa mmiliki wa fremu hizo kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini ambapo naye kwa upande wake alikuwa na haya ya kusema.


“Ni kweli hapo awali dada alimpangisha Wema hii fremu, lakini baadae kuna mambo yalitokea hivyo wakashindwa kuelewana, inasemekana kwamba Wema kodi ilimshinda ndio maana akaamua kuachia duka.


“Sasa kitu kizuri siku zote hujiuza, alipoondoka tu ndio Mobeto naye akahamia na sisi hatuwezi kukataa pesa kwa sababu tupo hapa kwa ajili hiyo,” alisema kijana huyo.


Kabla hawajaweka tofauti zao pembeni, Mobeto na Wema waliwahi kuwa kwenye bifu zito na hii yote ni kutokana na Mobeto kudaiwa kuwa kutembea na zilipendwa wa Wema Nasibu Abdul ‘Diamond’.Alipotafutwa Wema simu yake haikupatikana hewani hivyo atakapopatikana atafunguka kwa upande wake.

Post a Comment

0 Comments