TMA yasema kimbunga Jobo kitapiga mikoa minne nchini, Zanzibar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Aprili 25, 2021 Kimbunga Jobo kitapiga mkoani Dar es Salaam kikiambatana na upepo mkubwa wa  kilometa 60 kwa saa na kuleta madhara.
Mbali na Dar es Salaam, mikoa mingine itakayoathiriwa na kimbunga hicho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Unguja, Zanzibar eneo la Ziwa Victoria ambalo halitakuwa na athari ya moja kwa moja.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Aprili 23, 2021 na mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Dk Agness Kijazi akibainisha kuwa kwa sasa kimbunga hicho kipo kilometa 236 kutoka kisiwa cha Mafia kilichopo mkoani Pwani.

Amesema hadi Aprili 24, 2021 kimbunga hicho kitakuwa kilometa 126 kutoka kisiwa cha Mafia na Aprili 25, 2021 kitafika Dar es Salaam  kadri mwelekeo unavyoonyesha.

"Kulingana na ukubwa wa hiki kimbunga cha Jobo kina nguvu kadri  kinavyosogea nguvu yake inapungua lakini bado nguvu hiyo ni kubwa inaweza kuleta athari kwa sababu sasa hivi nguvu yake ni kilometa 90 kwa saa.”

"Lakini tunatarajia kwa kesho upepo utakuwa kilometa 70 kwa saa wakati kinatua Dar es Salaam kitakuwa kilometa 60 kwa saa ambao ni upepo mkubwa na unaweza kuleta athari. Sasa hivi kimeanza kushuka kinaenda kwa mwendo kasi kilometa 12 kwa saa lakini kinasogea  tahadhali ichukuliwe  kwa ukanda wa Pwani," amesema DK Kijazi.
________________

KISASI CHA USALITI PENZINI !!!,usipoipenda simulizi hii dai Mb na pesa zako,licha ya kuenjoy mahaba ndani yake kuna kitu cha kujifunza mwishoni Bofya Hapa kusoma Sehem ya 1 bure,sehem iliyobaki tsh 2000 kwa mtandao wowote.

Tembelea www.makapedia.com kwa stori mpya kila tarehe moja.


JE UNATAKA BIASHARA YAKO IWE YA UHAKIKA MIAKA YOTE YAJUE HAYA? usikose kitabu hiki Bofya Hapa kusoma sehem ya 1 bure sehem ya 2 tsh 2000 tu 

ndani ya www.makapedia.com

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad