Wakitaka kuniuza nipo tayari- Air Manula

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Bila kupepesa macho wala kung’ata maneno Mlindalango wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Klabu ya Simba Aishi Manula ndiye golikipa namba moja kwa hivi sasa nchini.



Na hili amedhihirisha katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika CAF, akiwa chini ya klabu yake ya Simba kwa kuwa na rekodi nzuri mpaka hivi sasa yakuto ruhusu magoli mengi na toka walipoanza michuano hiyo.

Simba ipo kwenye ‘MIKONO SALAMA’ chini ya Air Manula, wengine wanaweza kubisha lakini takwimu hazidanganyi.

Katika michezo minne (4) ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Mnyama Simba amecheza hadi hivi sasa hawajaruhusu goli hata moja hii inadhihirisha uimara wa Air Manula pale langoni ambaye ndiyo kipa alicheza dakika nyingi zaidi ukilinganisha na kipa mwingine ndani ya klabu hiyo.

Mechi nane (8) za Ligi hiyo ya Mabingwa inayokutanisha mabingwa tupu kutoka kwenye nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwa Simba SC nne (4) amecheza hatua za awali na nne (4) nyingine ikiwa ni hatua ya makundi na kufungukwa goli moja pekee kati ya hizo nane bao la Perfect Chikwende inatosha kumvisha taji Air Manula The Tanzania One kuwa ni namba mmoja nchini kwa sasa.

Ndani ya Taifa Stars katika mchezo wa mwisho aliyocheza ambao ulikuwa dhidi ya Libya, takwimu za Air Manula kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Aishi Manula

Minutes Played 93, Shots Saved 4, Super Saves 2, Shots Saved 100%, Passes 33, Accurate Passes 29, Accurate Passes 88%, Long Passes 6, Jumping Saves 3 na Close Range Shots 7. Hizi ni takwimu za Air Manula kwenye mchezo wake wa mwisho ndani ya Taifa Stars alipowakabili Libya Uwanja wa Mkapa jijini Dar Es Salaam.

Simba SC watamuuza Aishi Manula ?, taarifa zilizopo ni kuwa baadhi ya Klabu kubwa Afrika zimeanza kummezea mate mlindalango huyo wazamani wa Azam FC na wengine wapo tayari kuweka dau nono ili kunasa saini yake.

Kwa upande wake Aishi Manula yupo tayari na anausikiliza Uongozi wa Simba kama unampango wa kumuuza.

“Nashukuru kuwa mpaka sasa nimefanya vizuri na kuwa kipa namba moja Simba kwani wamepita makipa wengi kama akina Nduda, lakini hilo sasa ni la uongozi kwani wao wakitaka kuniuza sawa mie nawasikiliza wao tu” Alisema Manula.

Simba inatarajia kushuka uwanjani kuwakabili AS Vita Club Uwanja wa Mkapa huku Air Manula akitarajiwa kuimarisha vema milingoti mitatu siku hiyo kwenye mchezo muhimu mno.

IMEANDIKWA NA @fumo255

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad