5/08/2021

Barbara: Bila Kuifunga Yanga, Ubingwa Hautanoga

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amefunguka kuwa watafanya kila namna leo, Yanga afe pale kwa Mkapa kwani hakutakuwa na raha ya kuchukua ubingwa pasipo kumfunga mtani wao huyo.

 

Barbara alisema anaamini kwa asilimia 100 kuwa ushindi utapatikana kwani morali na ari ya wachezaji ipo juu sana na wao kama viongozi wameshamaliza majukumu yao, hivyo kilichobaki ni wachezaji kumaliza kazi ndani ya uwanja. 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Barbara alisema kuchukua ubingwa ukiwa umemfunga mtani kunakuwa na raha na furaha ya kitofauti, hivyo ubingwa wao wa msimu huu hautakuwa na maana kama watafungwa au kutoka sare na Yanga.

 

 

“Raha ya ubingwa ni kumfunga mtani, kutakuwa hakuna raha kama tutashindwa kuwafunga Yanga, binafsi naamini ushindi upo kwani ari na morali kwa wachezaji ipo juu sana na sisi viongozi tushakamilisha majukumu yetu,” alisema Barbara.

 

Leo Jumamosi Uwanja wa Mkapa utafunikwa na shangwe la jezi za njano na nyekundu pale ambapo Simba watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu ikiwa ni wa duru ya pili.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger