Billnass Amkana Nandy


BAADA ya mwanadada Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ kudai kuwa, staa wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘Billnass’ atakuwa mmoja wa washiriki wa Tamasha la Nandy Festival 2021, jamaa huyo ameibuka na kukana ishu hiyo.Kwa mujibu wa Nandy, Tamasha la Nandy Festival linatarajiwa kufanyika mikoa mitano nchini na katika Miji ya Mombasa na Nairobi nchini Kenya.

 

Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2019.Akizungumza alipokuwa anazindua msimu wa pili wa tamasha hilo, Nandy alisema kuwa, mwaka 2021 wanavuka mipaka na watakwenda nchini Kenya.“Tamasha litafanyika Nairobi na Mombasa, kwa Tanzania tamasha hili litafanyika mikoa mitano na Mkoa wa Kigoma ndiyo utakuwa fungua dimba, mikoa mingine tutaijua baadaye,” alisema Nandy.

 

Akizungumzia wasanii watakaoshiriki tamasha hilo, Nandy alisema ni wengi na miongoni mwao ni Billnass au Bilinenga au Nenga.“Billnass ni product (bidhaa) kwenye Nandy Festival hivyo mashabiki wategemee kumuona,” alisema Nandy.

 

Hata hivyo, katika mazungumzo na Gazeti la IJUMAA, Billnass amekana kuhusishwa kwenye ishu hiyo na kwamba hajui chochote juu ya tamasha hilo.Billnass amejibu kwa kifupi; “Sijui lolote juu ya Nandy Festival…”Miezi kadhaa iliyopita, uchumba wa Nandy na Billnass ulidaiwa kuyumba ambapo vyanzo vya ndani vinadai kuwa huwenda wakamaliza tofauti zao kupitia tamasha hilo


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE