Diamond Platnumz kutoa zawadi ya Eid Tandale


Mkurugenzi wa Makampuni ya Wasafi na Star wa Muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz anatarajia Kutoa alichojaliwa ikiwa kama zawadi yake katika Sikukuu ya Eid katika Maeneo aliyozaliwa na Kukua - TANDALE siku ya Kesho
Kupitia Ukurasa wake wa Twitter,Diamond Platnumz ameelezea namna ambavyo atarudi nyumbani kwao na Kushiriki sikukuu ya Eid na ndugu pamoja na watu wote wa karibu ambao wapo maeneo ya Tandale

Diamond Platnumz ameandika kuwa - Kesho InshaAllah baada ya sala ya Eid nitakuwa nyumbani Tandale nikitoa Mkono wa Eid kwa ndugu zangu Waislam..Zoezi hilo pia litafanyika Kariakoo likiongozwa na kaka angu Ricardo Momo..lakini pia Kilungule likiongozwa na Mkubwa fela, na Morogoro Mkuyuni likiongozwa na Boss Tale

Licha yaDiamond Platnumz kutoa Mkono wa Eid Tandale, pia Manager wake Mkubwa Fella atafanya hivyo hivyo kwa wakazi wa Kata ya Kilungule, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Babut Tale nae atashiriki kufanya tukio hili huko Morogoro Mkuyuni pamoja na Ricardo Momo kufanya hivyo kwa Wakazi wa Kariakoo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE