.

5/20/2021

Katibu Mkuu CCM Awaonya Wenye Nia Ovu Suala la Umeme
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaonya wale wote waliokua na nia ovu kwenye suala la umeme huku akiitaka Serikali kuwachukulia hatua za kisheria watakaothibitika kuhusika na jambo hilo.

 

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma ambapo ametoa maagizo kwa Serikali kupitia Wizara zake tatu.

 

Wizara ambazo Katibu Mkuu Chongolo amezitolea maelekezo ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Nishati.

 

Chongolo ameiagiza Serikali kupitia Wizara ya Nishati kuhakikisha inamaliza kwa wakati miradi yote ya Nishati ambayo imeanza kutekelezwa ukiwemo mradi mkubwa wa umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere uliopo Rufiji mkoani Pwani.

 

Katibu Mkuu Chongolo amesema kumalizika kwa mradi huo kutaongeza megawati za umeme zipatazo 2115 na kusaidia kuwa na umeme mwingi jambo ambalo litakuza uchumi wa Nchi kupitia viwanda.

 

“Nionye wale wenye nia ovu na nchi yetu ambao walitaka kutuweka gizani,niipongeze Serikali kwa hatua za awali walizochukua katika kuhakikisha wananchi wanaepukana na changamoto ya manunuzi ya umeme.

 

Lakini pia tunaiagiza Serikali kumalizia kuweka umeme vijiji ambavyo vimebaki kwani Ni vichache sana, lengo la Chama chetu ni kuona Nchi nzima inawaka umeme ili kuchochea kasi ya maendeleo kwa Taifa letu,” Amesema Chongolo.

 

Kuhusu Wizara ya Ardhi, Chongolo ameielekeza Wizara hiyo kuongeza kasi yake ya utoaji hati kwa wananchi katika kumiliki ardhi hatua ambayo itasaidia kuwafanya wananchi kuwa na usalama na ardhi yao.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger