Kesi ya Gugai Na Mwenzake Yakwama, Ni Baada ya Wakili Kuteuliwa kuwa Jaji

Kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zilizozidi kipato inayomkabili aliyekuwa mhasibu mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai na wenzake wawili imeahirishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kunatokana na wakili aliyekuwa anaendesha shauri hilo, Awamu Mbangwa kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Mbangwa alikuwa wakili wa Serikali mwandamizi  aliapishwa jana Ikulu Dar es Salaam na wenzake 27.

Taarifa ya kuahirishwa kwa Kesi  imetolewa na wakili kutoka Takukuru, Ipyana Mwakatobe wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka .

Mwakatobe amedai mbele ya  hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba kuwa Mbangwa sasa ni jaji na kuomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine.

“Kesi hii ilikuja kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji upande wa mashitaka lakini  aliyekuwa wakili mwenzangu, Awamu Mbagwa ameteuliwa kuwa jaji, hivyo naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji lakini pia kulipitia jalada husika kwa sababu kesi hii ilikuwa inaendeshwa na wakili mwingine” alidai.
Hivyo kesi imeahirishwa hadi Mei 31 mwaka huu.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE