Lil Wayne ashindwa kujizuia kwa Jay Z

 


Rapper Lil wayne ana tattoo iliyoandikwa 'Lucky Me' kwenye shingo yake chini ya sikio upande wa kushoto ikiwa ni heshima kwa Jay-Z kwa wimbo wake huo unao patikana kwenye album yake ya pili “In My Lifetime, Vol. 1”.

 

Albam hiyo iliachiwa chini ya Roc-A-Fella Records kwa kushirikiana na Def Jam Recordings Novemba 4, 1997.


Sio shingoni tu, kwani Lil tunechi pia amejichora verse nzima ya wimbo huo kwenye moja ya mguu wake na ikumbukwe kwenye moja ya mahojiano yake, Wayne aliwahi kusema aliacha kusikiliza muziki wa wasanii wengine baada ya Jay-Z kuiachia album yake, The Black Album mwaka 2003.


Tunechi ana tattoo zaidi ya 89 mwilini mwake zikiwa na maana yake

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE