"Mapenzi kwanza sio pesa" - Vera Sidika

 


Kutoka 254 Kenya mrembo Vera Sidika amesema hana ndoto ya kuolewa na mwanaume Milionea, Bilionea au tajiri ndio maana hata ukimuwekea mapenzi na pesa basi atachagua upande wa mapenzi kwanza.

Vera Sidika amejibu hilo baada ya kuulizwa na shabiki kupitia 'Insta Story' ambapo alitoa nafasi kwa mashabiki kumuuliza swali lolote wanalojisikia, shabiki huyo aliuliza kwamba "utaenda kwenye pesa au mapenzi".


"Nitachagua mapenzi kila wakati, tangu kitambo sijawahi kuwa msichana mwenye ndoto ya kuolewa na Milionea, Bilionea au tajiri mimi sio mtu wa aina hiyo ninachokitaka kutoka kwa Baby wangu ni mapenzi" ameeleza Vera Sidika


Vera Sidaka kwa sasa yupo kwenye mahusiano na msanii Brown Mauzo awali aliwahi ku-date na mtanzania Jimmy Chansa.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE