Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mbelgiji: Simba Ikiifunga Yanga Kwisha Habari Yao

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURELUC Eymael, raia wa Ubelgiji, kocha wa zamani wa kikosi cha Yanga, amesema kuwa ikiwa timu hiyo itafungwa na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8 habari ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara inaweza kuishia hapo.

 

Eymael alifutwa kazi ndani ya Yanga kwa kile kilichoelezwa kuwa ni lugha ya ubaguzi wa rangi jambo ambalo alilipinga.Akizungumza na Championi Jumamosi, Eymael ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji alisema kuwa anaifuatilia ligi ya Tanzania kwa ukaribu na anatambua kwamba mchezo wa Simba dhidi ya Yanga utatoa picha ya bingwa.

 

“Najua kwamba Yanga watacheza na Simba mchezo wao ujao wa ligi na ikitokea wakifungwa basi safari yao ya kutwaa ubingwa msimu huu itakuwa ngumu kwa kuwa kama Simba watashinda mechi zao ambazo wapo nazo mkononi inakuwa ni fursa kwao kuweza kushinda taji hilo.“

 

Nimeifundisha Yanga na ninajua namna ilivyo, kwangu bado ninahesabu mafanikio makubwa ambayo niliweza kufanya ni kuitoa timu kutoka nafasi ya sita mpaka nafasi ya pili, pia kuifunga Simba baada ya muda wa miaka mitano,” alisema Eymael.

Post a Comment

0 Comments