.

5/24/2021

Mfahamu Hoyce Temu
UNAAMBIWA kuwa Hoyce Temu alisoma Stashahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Mahusiano ya Kigeni yaani Post Graduate Diploma in Management of Foreign Relations (PGD-MFR) kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini Dar es Salaam ama Mozambique-Tanzania Centre for Foreign Relations (CFR).

 

Lakini pia wengi huenda hawafahamu kuwa Hoyce Temu aliwahi kuhudumu Umoja wa Mataifa Tanzania (UN-Tanzania) kama Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano lakini pia alipata kuhudumu kama Mtaalamu wa Mawasiliano UN-Tanzania (UN Communication Specialist) na pia Mchambuzi wa Mawasiliano au UN Communication Specialist.

 

Hivyo Hoyce Temu ana taaluma ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia na zaidi ya hilo ana weledi wa masauala ya kidiplomasia kutokana na kufanya kazi UN ofisi ya Tanzania.

 

Alichosoma Hoyce Temu ndicho walichosoma maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao kikanuni ni lazima wasome kozi za Chuo cha Diplomasia (CFR) kama kigezo kimojawapo cha kutoka ngazi moja ya daraja kwenda lingine ili waweze kumudu majukumu yao ipasavyo.

 

Hayo na mengine mengi huzingatiwa pia katika uteuzi wa wale wanaotokana na weledi (Career Diplomats) kama vile kujaza nafasi za ukurugenzi katika idara zilizopo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, baadhi vituo (balozi zilizopo nje) kuwa wazi, wapo mabalozi waliomaliza muda wakijiandaa kurudi, kuna kubadilishwa vituo vya kazi na majukumu mengine nchini kwa kadiri Rais atakavyoona inafaa.

 

Hawa wanaotokana na weledi ni wale ambao wametokea wizara ya mambo ya nje ambao huwa wanapatikana kutokana na kukua katika kazi ama career growth.

 

Kwa mfano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (MFAEAC) ya Tanzania afisa wa Wizara wa Wizara ya Mambo ya Nje (FSO) huwa na mtiririko ufuatao wa ajira kuanzia tangu afisa anaajiriwa mpaka anafikia hatua ya kuteuliwa kuwa Balozi.

 

Mtu anapoajiriwa katika Wizara ya Mambo ya Nje huanza na cheo cha Third Secretary (TS) cheo hiki katika mfumo wa utumishi (Scheme of Service) hujulikana kama Afisa Mambo ya Nje daraja la Tatu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger