Mwanamke Azua Gumzo, Aweka Nyoka Kwenye Jeneza la Mumewe
MWANAMKE mmoja kutoka Ghana amezua hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye video akiweka nyoka ndani ya jeneza la mumewe.

 

Iliripotiwa kuwa mwanamke huwa alikuwa ameghadhabishwa na waliohusika na kifo cha mumewe na alitaka wapate adhabu kali.

 

Kwenye video hiyo ambayo imesambaa mitandaoni, mwanamke huyo alidai kwamba mumewe aliuawa kwa kuumwa na nyoka kwenye ulimi na anaamini kuna watu walipanga njama hiyo.

 

Ilisemekana kwamba jamaa huyo aliuawa kwa kuumwa na nyoka kwenye ulimi kwa hivyo mkewe akamua kumzika nayo ambapo kulingana na mila, mwanamke huyo alifanya hivyo ili nyoka huyo akabiliane na wale waliohusika na kifo cha mumewe.

 

Video hiyo iliibua hisia tofauti miongoni mwa wanamitandao baadhi ya maoni;

@funghana_ Alisema inaaminika kwamba jamaa huyo aliuawa, kwa hivyo nia yake kuwekewa nyoka ilikuwa ni kukabiliana na waliohusika na kifo chake.

@bby__naa.” Naye alisema .“Hii ni kama kukiuka haki za nyoka , wao pia wana haki zao”

@cabi_diana: “Haya ni maajabu.

” @wurdzfreeman “Ati aliumwa na nyoka kwa ulimi? kivipi na inawezakanaje?”

@ericaabyna: “Eish, hii inamaanisha nini?”

@jerryjustice: “Aaah, Hii ni nini sasa?”

@1plus1builders: “Hii ni muvi ama nini?”

 


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE