.

5/21/2021

Mwarabu Fighter kuwa Bodyguard wa Alikiba?

  


Bodyguard maarufu wa wasanii Mwarabu Fighter amesema anamuheshimu msanii Alikiba na wakikutana pamoja hawezi kuwa mbali nae kwa sababu watu wanamfahamu kwa kazi ya ulinzi hivyo si vyema ikitokea jambo baya kwa msanii huyo wakati yeye yupo.


Mwarabu Fighter amejibu hilo kupitia EATV & EA Radio Digital kufuatia picha inayomuonesha anamlinda Alikiba na watu kutafsiri mitandaoni kwamba tayari amekuwa bodyguard rasmi wa Alikiba.

"Alikiba ni msanii mkubwa ukizingatia kazi yangu iliyonitambulisha ni ulinzi, lakini ninapomkuta msanii mkubwa kama yeye katika kundi langu namuheshimu, ile picha tulikuwa kwenye msafara mmoja wa mabalozi, kwa hiyo kwa ukubwa wake siwezi kukaa hatua 100 na yeye" 

"Lazima niwe karibu hata ikitokea mtu ghafla akam-block nimzuie, na ilinilizamu kuwa karibu vile ili hata likitokea la kutokea kama shabiki kumdhuru halafu mimi nipo pale isingekuwa vizuri, watu wangeandika vibaya kwamba tukio lile linatokea wakati mimi nipo" ameongeza Mwarabu Fighter 


Swali lililopo ni kwamba Mwarabu Fighter anaweza akawa Bodyguard wa msanii Alikiba, majibu kamili mtazame hapa chini akizungumzia hilo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger