.

5/27/2021

Rasmi Zidane aondoka Real Madrid

Klabu ya Real Madrid ya Hispania imethibitisha kuwa Kocha Zinedine zidane amejiuzulu nafasi yake ya ukocha ndani ya kikosi hicho, hivyo sio Kocha tena wa klabu hiyo.
Taarifa hii ya kujiuzulu kwa zidane kama kocha mkuu wa Los Blancos inafuatia baada ya kikosi hicho kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya majirani zao kutoka katika jiji la Madrid klabu ya Atletico Madrid.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia tovuti yao imesema. Zinedine Zidane ameamua kuachia nafasi yake kama kocha mkuu wa klabu yetu, sasa ni wakati wa kuheshimu uamuzi wake na kumwonyesha shukrani zetu kwa weledi wake, kujitolea na mapenzi kwa miaka yote.

Zidane mwenye umri wa miaka 48 ameifundisha Real Madrid katika vipindi viwili tofauti, awamu ya kwanza ilikuwa kati ya Januari 4, 2016 mpaka Mei 31, 2018, ambapo alikiongoza kikosi hicho kwenye michezo 149 na kushinda jumla ya mataji 9 ikiwemo ubingwa wa ligi kuu Hispania La Liga na alitwaa ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya mara 3 mfululizo.

Na alirejea kwa mara ya pili ambapo alitwaa tena mikoba ya kukinoa kikosi hicho cha mabingwa wa kihistoria barani kuanzia Machi 11 2019 mpaka leo Mei 27, 2021 na katika awamu hii amefanikiwa kushinda mataji mawili tu, iliwemo ubingwa wa Ligi Kuu ambao alishinda msimu uliopita, na amekiongoza katika michezo 114.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger