.

5/23/2021

SGR Dar- Moro Kuanza Agosti 2021


MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema shirika hilo litaanza majaribio ya safari za treni za mwendo kasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro Agosti mwaka huu.


Akizungumza na Rais Samia Suluhu, Ikulu jijini Dar es Salaam, Kadogosa alisema ujenzi wa mradi huo katika kipande cha Dar es Salaam—Morogoro chenye urefu wa kilometa 300 umefikia asilimia 91 na unaendelea vizuri.Ujenzi kipande cha Morogoro-Makutupora chenye urefu wa kilometa 422 umefikia asilimia 60.02. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Kadogosa amemshukuru Rais Samia na serikali ya Awamu ya Sita kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 372.34 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande cha tano cha reli ya Mwanza-Isaka chenye urefu wa kilometa 341 kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge Raiway-SGR).Rais Samia alisema serikali imedhamiria kuhakikisha ujenzi wa reli ya kati utakaounganisha bandari ya Dar es Salaam na mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi unakamilishwa ili kuzifikia nchi za Uganda, Burundi, Rwanda na DRC.Alimtaka Mkurugenzi huyo Mkuu wa Shirika la Reli kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ya ujenzi vizuri ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa ajili ya ujenzi wa vipande vua Makutopora-Tabora, Tabora-Isaka na Kaliua-Mpanga-Kalema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger