.

5/21/2021

Yanga Watoa Kauli Kuhusu Ubingwa VPL

NAHODHA msaidizi wa kikosi cha Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa licha ya timu hiyo kuwa na matokeo yasiyotabirika katika michezo ya hivi karibuni, bado hawajakata tamaa katika malengo yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.

 

Yanga, juzi Jumatano waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na kufi kisha pointi 61, hivyo kuwafi kia vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ambao wamejikusanyia pointi 61 licha ya kuwa na michezo minne pungufu dhidi ya Yanga.

 

Yanga wamekuwa na mwenendo wa kusuasua ambapo katika michezo nane mfululizo iliyopita wamefanikiwa kushinda michezo mitatu pekee, wamepoteza miwili na kutoa sare kwenye tatu.Matokeo hayo yameonekana kuzidi kuwapunguza kasi Yanga katika vita ya kuwania ubingwa wa msimu huu.

 

Akizungumzia mipango yao Mwamnyeto alisema: “Ni kweli tumekuwa na mwendo wa kusuasua kwenye michezo yetu iliyopita, lakini tunaamini kuwa hiyo ni hali ya kawaida na ni suala ambalo tayari linafanyiwa kazi na benchi letu la ufundi.“

 

Hivyo, tunapambana kuhakikisha tunafi kia malengo yetu msimu huu ikiwemo kumaliza katika nafasi za juu, na hata kutwaa ubingwa.”Naye Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli akizungumza na Championi Ijumaa, alisema:

 

“Tunaendelea kujenga kikosi chetu, lakini pia tunaendelea kupigania malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu, changamoto ya matokeo ni kitu cha kawaida na hatuwezi kukata tamaa.”Yanga watoa kauli kuhusu ubingwa VPL

STORI: JOEL THOMAS, Dar es Salaam

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger