Afrika yakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya Covid-19

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Afrika inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona, wakati hospitali zikiendelea kuwapokea wagonjwa na vifo vikishuhudiwa, hali ambayo imechangia vituo vya afya kuzidiwa, huku bara hilo likiwa nyuma katika kampeni ya chanjo ya ulimwengu. 
Janga la corona limetajwa kuibuka tena kwa kiwango cha kutisha katika nchi zisizopungua 12, huku visa vya maambukizi vikitarajiwa kufikia rekodi ya juu ndani ya wiki tatu. 

Mkurugenzi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Afrika CDC, John Nkengasong, ameelezea wimbi la tatu kuwa baya sana. 

Hadi kufikia sasa, kirusi cha Delta kilichogunduliwa mara ya kwanza nchini India, kimeripotiwa katika nchi 14 za Afrika. 

Idadi kubwa ya maambukizi imeshuhudiwa katika nchi za Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Afrika imeorodhesha maambukizi chini ya milioni 5.3 na vifo ni 139,000.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad