Yanga Yatinga Fainali ya Kombe la Shirikisho

TIMU ya Wananchi Yanga Imefanikiwa kutinga Hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup) baada ya kuitungua Biashara United kwa bao 1-0, kwenye mchezo uliochezwa Leo Juni 25, kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

 

Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo limefungwa na Yacouba Sogne dakika ya 22 ya mchezo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Feisal Salum ‘Fei Toto’.

 

Mara ya mwisho Yanga kucheza fainali ya michuano hii ilikuwa msimu wa 2015-16 ambapo waliibuka mabingwa kwa kuifunga Azam FC, mabao 3-1.Kwenye mchezo wa fainali timu ya Wananchi watacheza na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya Pili itakayo chezwa kesho Juni 25, 2021, huko Songea mkuani Ruvuma kwenye uwanja wa Majimaji ambapo Mabingwa watetezi Simba Sc watakuwa wakicheza na Azam FC.

 

Mchezo wa fainali ya michuano hii msimu huu 2020/21 utachezwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad