.

6/07/2021

Mrithi wa Carlinhos Aanza Kusakwa Yanga
UONGOZI wa Yanga, umeweka wazi kuwa, utaingia chimbo kumtafuta mbadala wa nyota wao, Carlos Carlinhos, raia wa Angola ambaye hivi karibuni aliomba kuvunjiwa mkataba wake.

 

Carlinhos ambaye alisaini dili la miaka miwili kuitumikia Yanga, aliomba kuvunja mkataba wake na timu hiyo Mei 31, mwaka huu, na tayari ameondoka.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema kwa sasa hesabu zao ni kuona namna gani wanaweza kumpata mchezaji mwingine watakayemsajili kuchukua nafasi ya kiungo huyo.

 

“Tumekubaliana na Carlinhos kwa uzuri na tumeona kwamba tubaki huru kwa sasa na kumtafuta mchezaji mwingine kwenye dirisha la usajili kama itafaa.

 

“Tunamshukuru kwa alichokifanya Yanga, mabao matatu na pasi zake si haba. Naona wengi wanazungumza kuhusu mapokezi yake, wanasahau kwamba ulikuwa ni mkakati wetu.

 

“Tulikuwa na mkakati wa kimasoko na tulikuwa tumetoka kwenye janga la Covid-19, tuliamua kufanya mapokezi yale yawe ya wazi ili kutengeneza hamasa. Watu wasichanganye mambo, ule ulikuwa mpango maalumu na tulifanikiwa kwani mauzo ya jezi yalikuwa makubwa,” alisema Bumbuli.

STORI; LUNYAMADZO MYUKA, DAR ES SALAAM

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger