.

6/08/2021

Rais Samia "Watoto wa kiume wapo faster kidigitali kuliko Wanawake, Nikikwama Kitu Kwenye Simu Nampa Mjukuu Wangu Ibra Anisaidie"

 


“Kwenye mambo ya kidigitali Wanawake bado, Wanaume leo wengi wamejiajiri kupitia mifumo ya kidigitali ila Wanawake ni kuuza nyanya na michicha kwenye digitali wapo wachache sana, lazima tuzibe pengo hili, Dunia sasa inaendeshwa kidigitali”———Rais Samia akizungumza na Wanawake Dodoma leo

“Kuna pengo la kidigitali kwa Wanawake, hata Mimi nikikwama kitu kidogo kwenye simu yangu nina kajukuu kangu kanaitwa Ibra ana miaka 9 anaichukua anaitazama dakika chache anasema Bibi tayari lakini nina Kajukuu kanaitwa Samia ukimpa angalia anasema sijui mpe Ibra”———Rais Samia

“Hata kwa Familia zetu Watoto wa kiume wapo faster kidigitali kuliko Wanawake ndio maana tukaweka Shule za kufundisha Wasichana Sayansi ili tuzibe pengo hili la kidigitali kwa Wanawake”———Rais Samia

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger