Sure Boy Basi Tena Yanga, Asaini Azam FC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





KIUNGOmchezeshaji fundi, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ ataendelea kuichezea Azam FC katika misimu mingine miwili baada ya kuongezewa mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kukipiga huko.

 

Awali, ilielezwa kuwa kiungo huyo yupo kwenye mipango ya kujiunga na Yanga katika msimu ujao kwa kile kilichodaiwa kugomea kuongeza mkataba Azam.

 

Taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kiungo huyo ameongeza mkataba wa miaka miwili kwa siri katika timu yake ya Azam utakaomalizika msimu wa 2023.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa wamemuongezea kiungo huyo mkataba kwa makusudi kwa hofu ya kuzidiwa ujanja na baadhi ya klabu kubwa za Simba na Yanga.

 

“Kama kulikuwa kuna timu ilikuwa inavizia saini ya Sure Boy, basi imekula kwao kwani mchezaji huyo ni mali yetu kwa misimu mingine miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.Alipotafutwa Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zakaria kuzungumzia hilo alisema: “Mbona mmechelewa kujua taarifa za Sure Boy kuongeza mkataba mpya? Sure ni mali yetu yupo hapa Azam hadi 2023.”

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

 
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad