Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Hizi Ndio Shule 10 Bora Matokeo Kidato cha Sita 2021
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 na kutaja shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 10, 2021 visiwani Zanzibar wakati akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 72.

Msonde amesema Kemebos ya Kagera yenye watahiniwa 35 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Dareda ya Manyara watahiniwa 101. Nafasi ya nne amsema imechukuliwa na Tabora Girls yenye watahiniwa 100 ikifuatiwa na Tabora Boys yenye watahiniwa 120.

Nafasi ya sita imeshikwa na Feza Boys ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na watahiniwa 71 ikifuatiwa na Mwandet ya Arusha yenye watahiniwa 53.


 
Zakia Meghji imeshika nafasi ya nane ikitokea mkoani Geita. Ilikuwa na watahiniwa 31, ikifuatiwa na Kilosa ya Morogoro yenye watahiniwa 91, na Mzumbe watahiniwa 135.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

1 Comments

Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)