Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Watu 408 Wana Corona Tanzania, 284 Wanapumulia MashineWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi kufikia Julai 8, 2021 jumla watu 408 walibainika kuwa na ugonjwa wa corona huku 284 wakitumia mitungi ya oksijeni.

Dk Gwajima ametoa taarifa hiyo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwenye mnada wa Msalato jijini Dodoma.

Kwa upande wa Mkoa wa Dodoma, Waziri huyo amesema hadi kufikia Julai 8, 2012, jumla ya watu 26 waligundulika kuwa na ugonjwa huo huku 22 wakiwa katika mitungi ya oksijeni.

Wakati huo huo, Dk Gwajima na kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka wametembea umbali wa kilometa nne lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kuvaa barakoa ili kujikinga na maambukizi.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments