Mangungu Awataka Wanasimba Kuwa Watulivu Kuhusu Haji Manara na Barbara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amewataka wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuwa watulivu kuhusu yanayoendelea kati ya Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Msemaji Haji Manara na kuwahaidi kuwa baada ya mashindano, tathmini ya mwenendo mzima wa timu na watendaji wake itafanyika
Kauli hiyo imekuja baada ya msemaji wa klabu hiyo Haji Manara kumtuhumu Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kumfanyia chuki na kumtuhumu kuihujumu timu.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagramu Murtaza Mangunguameandika;

Wana Simba tuwe watulivu

Ninawaomba sana wanachama, wapenzi na washabiki wa Simba tuwe watulivu na makini kuelekea fainali ya FA CUP.

Uongozi wa Simba upo nakini na ulishatoa maelekezo ya kutatua mgogoro uliojitokeza.

Simba ni timu inayojipambanua kuendeshwa kiweledi, hivyo tusimame katika misingi hiyo.

Wote wanaolumbana ni waajiriwa na muajiri yupo.

Baada ya mashindano, tathmini ya mwenendo mzima wa timu na watendaji wake itafanyika.

Kwa sasa kila mmoja wetu azingatie nidhamu,hekima na misingi ya ajira au nafasi yake katika club.

Nawaomba tuwe watulivu na tuendelee na mikakati ya michezo ijayo.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad