.

7/31/2021

Mmiliki wa Peacock Hotel afariki duniaDar es Salaam. Mmiliki wa hoteli ya Peacock, Joseph Mfugale amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa ndugu za Mfugale aliyetajwa kuwa msemaji wa familia, Expedito Mfugale alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alisema hawezi kuzungumzia.


Hata hivyo, mmoja wa ndugu zake ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini kwa kuwa si msemaji wa familia, anasema Mfugale amefariki le Julai 31 asubuhi na msiba uko nyumbani kwake Kibamba Dar es Salaam.


“Ni kweli kaka amefariki leo asubuhi. Alikuwa anaumwa, muda mrefu, lakini swali kwamba alikuwa anaumwa nini ni la kifamilia,” alisema ndugu huyo.


 

Mfugale ni miongoni mwa wamiliki wa hoteli wazawa aliyepata mafanikio katika biashara hiyo, akifungua hotel Dar es Salaam na nyingine mkoani Iringa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger