Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mzee Mpili Augua Ghafla Dar
HAJI Omari ‘Mzee Mpili’ amezua hali ya sintofahamu, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa kifua.Mzee Mpili aliugua ghafla juzi Jumatano akiwa nyumbani kwake Ikwiriri, wilayani Rufiji, Pwani, lakini kesho yake alipata nguvu ya kufuata milioni yake aliyoahidiwa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kama Yanga ikiifunga Simba.

Kweli jana Alhamisi alichukua mzigo wake huo na kurejea zake Ikwiriri ambako inaelezwa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

Mzee huyo alijipatia umaarufu mkubwa katika mchezo kati ya Simba na Yanga, baada ya kudai kuwa ‘aliutengeneza’ mchezo huo kwa faida ya Yanga, na kweli wakashinda 1-0 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Mzee Mpili, Mohamed Mkilalu, alisema kuwa: “Mzee amerejea leo (jana) Ikwiriri baada ya kwenda Dar kuchukua fedha zake kwa Haji Manara.


 
“Manara alimpa ahadi ya milioni moja endapo Yanga itaifunga Simba, kwa hiyo alimkodia usafiri wa kwenda na kurudi.“Ni kweli alikuwa anaumwa kifua lakini sasa hivi anaendelea vizuri baada ya kutumia dozi ambazo amepewa na daktari.”


 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments