.

8/07/2021

Breaking: Karia Aidhinishwa Kuiongoza Tena TFF Miaka Minne
Wallace Karia leo Agosti 7, 2021 amepitishwa na wajumbe wote 81 kuwa Rais mteule wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

 

Karia amepitishwa kwa sababu ni jina lake pekee lililopitishwa katika mchujo wa wagombea ambao walichukua fomu kuwania nafasi hiyo.

 

Wajumbe walikuwa na kazi ya kuidhinisha jina lake leo  katika uchaguzi ambao unafanyika leo Tanga.

 

Kwa mujibu wa ibara ya 19 ya sheria ya uchaguzi ambayo inasema wajumbe watapiga kura za ndiyo au hapana kwa mgombea yeyote ambaye atakuwa peke yake.

 

Mbali na nafasi ya Urais pia kuna nafasi za Wajumbe ambao wapo 17 hawa watapigiwa kura kutokana na kanda zao ambazo wapo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger