DC Joshua Nasari Akabidhiwa Ofisi na Wadau wa Maendeleo, Bunda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Bunda, Mara. Siku ya Tarehe 8/8/2021 Kundi la wadau wa maendeleo mkoa wa Mara wanaoishi na kufanya kazi sehemu mbalimbali hapa nchini (Mara Investors) limekabidhi jengo kwa ajili ya ofisi ya Serikali ya Mtaa ili kusaidia huduma za kiutawala kwa wakazi wa mtaa wa Serengeti Kata ya Nyatwali Bunda mjini.


sehemu ya muonekano wa ofisi hiyo.

 

 

Jengo hilo lenye thamani ya Shilingi milioni 15.5, limejengwa kwa msaada wa wadau wa maendeleo wa mkoa Mara ikiwa ni Pamoja ,Dkt. Amon Manyama, Dkt. Sebastian Ndege na Wakili Deus Mgengeli.


DC Nasari akisikiliza maelekezo kutoka kwa Dkt Sebastian Ndege (aliyenyoosha mkono) ambaye ni mmoja wa wadau walichangia ujenzi wa ofisi hiyo.

 

 

Wadau hao wamejitolea kujenga ofisi hiyo ili kusaidia upatikanaji wa huduma za Kiserikali katika ngazi ya mtaa kutokana na mahitaji yanayokuwepo kwa Muda mrefu. Pia linatarajiwa kuwa kituo cha taarifa mbalimbali za kitalii na uwekezaji katika eneo la Nyatwali,Bunda.

 

 

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi jengo hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nasari aliwashuru wafadhili hao na kuwataka wakazi wa Bunda kupokea kwa mikono miwili ofisi hiyo na kujipanga kwa kumalizia kuongezea kile kilichopungua kwenye ofisi hiyo.

 

Nasari alisema ofisi hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa pamoja na kutoa huduma za kiserikali kwa wananchi wa eneo hilo, pia itatoa huduma ya taarifa za utalii hususani katika ukanda wa Magharibi mwa Serengeti.

 

Mkuu huyo wa wilaya aliwashukuru Mara Investors kwa kujitolea kujenga ofisi hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza katika kusaidia jamii kupambana na changamoto mbalimbali ili kuweza kupata maendeleo.

 

Sekta binafsi ni wadau wetu katika maendeleo ya nchi kwa ujumla,Serikali pekee haitoweza kufanikisha. Na nyie wananchi muunge mkono juhudi za serikali kwa kuchapa kazi, kupiga vita uzembe na tabia za umbea na uzururaji ”Alisema Ndugu Nasari.

 

Pamoja na kushiriki kuzindua ofisi hiyo Nasari hiyo alipata fursa ya kupanda miti kadhaa ikiwa ni ni sehemu ya uhamasishaji wa kutunza mazingira wilayani humo.

 

Kwa upande wake, Dkt Amon Manyama, mmoja wafadhili waliochangia ujenzi huo, alisema yeye pamoja na wenzake wamejipanga kwa ajili ya kusaidia kufikisha huduma ya maji na umeme pamoja na miundombinu ya taa za kutumia umeme wa jua (solar) ili kuimarisha na kusaidia shughuli za kiuchumi na kijamii katika eneo la Ndabaka Centre.

 

Naye mwekezaji kutoka Jembe Group Dkt. Sebastian Ndege aliiomba serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kusaidia uwekezaji wenye tija unaofanywa na sekta binafsi.

 

Aidha Dkt Ndege aliahidi kuendelea kusaidia jitihada mbali mbali za kimaendeleo katika mtaa wa Serengeti kwa kufadhili Ujenzi gati ya Maji safi na Salama na choo cha kisasa kwa ajili ya wageni na watalii wanaopita eneo hilo.

 

Aidha amewataka uongozi wa Wilaya kunadili matumizi ya soko lililojengwa hapo na kuwa gofu,litumike kama soko la kitalii ambapo litatoa ajira kwa vujana na kina mama wa Mtaa huo.

 

Mwekezaji mwingine kutoka Mara Investors Wakili Deogratius Mgengeli aliiomba serikali kushughulikia kero ya umiliki wa ardhi kupitia Hati za kimila ili ziweze kutumika kupata mikopo ya uwekezaji katika eneo hilo.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad