.

8/16/2021

Gomes: Tutarudi Tukiwa Vizuri

 


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa watareja Tanzania wakiwa vizuri kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za kimataifa ambapo timu hiyo inawakilisha Tanzania kwenye ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Kwa sasa Simba imeweka kambi nchini Morocco ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao wa 2020/21 ikiwa imeanza kazi na majembe mapya ambayo ni pamoja na Peter Banda, Pape Sakho.

 

Ina kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara ambalo ilitwaa msimu uliopita pamoja na Kombe la Shirikisho na kwenye hatua ya Ligi ya Mabingwa iliishia hatua ya robo fainali.

 

Gomes alisema kuwa wanatambua msimu ujao wana kazi kubwa ya kufanya lakini watapambana ili kuweza kupata matokeo mazuri hasa kwa maandalizi ambayo wanayafanya.

 

“Tunafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya msimu ujao, kwa namna ambavyo wachezaji wanajituma na uwezo wao nina amini kwamba tutarudi msimu mpya tukiwa imara,” alisema Gomes.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger