.

8/02/2021

Jay Melody aogopa lawama za Alikiba na Rayvanny

 


Hitmaker wa ngoma ya najieka na huba hulu Jay Melody amesema kumekuwa na shida ya kuachia remix ya huba hulu kwa sababu hataki kuonekana kutengeneza mashindano baina ya Alikiba na Rayvanny ambao walitaka kufanya remix hiyo.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Jay Melody anasema Alikiba na Rayvanny wana timu tofauti jambo ambalo linaweza kusababisha remix hizo zisitoke au kutoka kama itawezekana.

"Remix zilikuwa na shida kutoka japo nipo kwenye mipango kama zinaweza kutoka lakini kwa bahari mbaya zinaweza zisitoke, shida ilikuwa kwangu kwa sababu sitaki kuonekana mtu ambaye natengeneza  'competition' ya watu wawili au kuwa kati ya mpambano hizo ni timu mbili tofauti" ameeleza Jay Melody

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger