.

8/02/2021

Mbaroni kwa kumuua baba yake na kumzika kimya kimya
Polisi Mkoa wa Rukwa inamshikilia kijana mmoja (35) mkazi wa Kata ya Chanji kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi, Thomas Mremi (85) na kumzika kimyakimya nyumbani kwao.

Mremi, aliyekuwa ofisa mstaafu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza aliyestaafu utumishi wa umma akiwa na cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP), aliuawa usiku pasipo watu kufahamu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, William Mwampaghale alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo juzi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.

Alisema mtuhumiwa, ambaye hakumtaja jina kwa kuwa uchunguzi unaendelea, anadaiwa kumuua baba yake huyo kwa kumpiga kichwani na kitu kizito katokana na kuwepo kwa mzozo wa muda mrefu kati yao, ambapo mtoto huyo alitakiwa kuondoka nyumbani na baba yake kwa sababu amefikia umri wa kujitegemea.  #MwananchiUpdates

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger