.

8/24/2021

Mbowe Agoma Kutoa Maelezo

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo Agosti 23, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa maelezo ya mashtaka mbalimbali yanayowakabili ikiwemo la kutaka kudhuru viongozi wa serikali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

 

Mahakama hiyo imeelezwa na upande wa mashitaka kuwa, mshtakiwa namba nne katika kesi ya uhujumu uchumi na kupanga njama ugaidi, Freeman Mbowe, amekataa kutoa maelezo yake polisi badala yake amesema atayatoa mahakamani.

 

Washatakiwa wenzake watatu wameieleza Mahakama hiyo kuwa, maelezo yaliyosomwa na upande wa mashitaka, yakidaiwa ya kwao, waliyatoa bila hiari yao baada ya kulazimishwa kusaini kwa kupigwa. Mbowe aligoma kutoa maelezo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger