.

8/15/2021

Mvua ya barafu yaharibu mazao, nyumba Biharamulo
Mvua ya upepo na barafu iliyonyesha wilayani Biharamulo    Mkoa wa Kagera juzi imeharibu mazao na nyumba na kuacha barafu katika makazi.


Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumamosi Agosti 14, 2021 Diwani wa Biharamulo Mjini, David Mwenenkunda  amesema mvua hiyo iliyonyesha jana jioni kuanzia  saa nane  mchana hadi saa kumi jioni imeacha madhara kwa wakazi wa kata hiyo nyumba zao kuharibika kwa kujaa maji na barafu."Mpaka sasa upepo ulikuwepo lakini hakuna nyumba iliyoezuliwa, zimetoboka kwenye kuta kwa sababu ya mawe ya mvua,"amesema Mwendankunda.Ametaja maeneo yaliyoathirika ni mitaa ya Lubondo na Lukaragata ambayo mpaka sasa barafu bado hazijayeyuka kuisha licha ya uwepo wa jua.


Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Kemilembe Lwota amesema mvua hiyo imenyesha na baada ya wananchi kutoa taarifa ametembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua hiyo.

Amesema mvua hiyo haijasababisha madhara makubwa kwa wananchi zaidi ya kuwepo barafu kwenye maeneo yao.


Shuhuda wa tukio hilo  Sadoth Trazias amesema lilikuwa tukio  la kushangaza kutokana na mvua hiyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger